Kurasa Zangu (Mina Sidor)
Kurasa Zangu (Mina sidor) ni mahali ambapo unaweza kufuatilia nyumba ambazo umeandikisha kuvutiwa nazo. Pia utapata habari kuhusu muda wako wa foleni na ada ya kila mwaka, na unaweza kusasisha maelezo yako ya kibinafsi hapa. Utahitaji kuingia kwenye akaunti yako ili kufikia Kurasa Zangu.
Kuingia kwenye akaunti
Njia rahisi na salama ya kuingia ni kutumia mfumo wa utambulisho wa kielektroniki wa BankID (Bank-ID). Ikiwa huwezi kupata BankID, unaweza kuunda akaunti ambayo inakuruhusu kuingia ukitumia anwani yako ya barua pepe na neno siri.
Ingia kwenye akaunti ili kufuatilia:
Vyumba maalum ambavyo unaweza kuandikisha kuvutiwa kwako.
Nitasubiri muda gani kwenye foleni?
Simamia maombi yako. Maombi ya sasa na ya zamani.
Ada ya mwaka – je, imelipwa?
Unaweza pia kusasisha maelezo yako ya mawasiliano ili tuweze kuwasiliana nawe kwa urahisi.
Mwaliko wa ukaguzi
Ikiwa una moja ya nyakati ndefu zaidi za foleni za watu ambao wameandikisha kuvutiwa na nyumba fulani, tutakutumia mwaliko wa kukagua nyumba. Maelezo yote ya ukaguzi yanapatikana kwenye Kurasa Zangu. Baada ya kukagua, utahitajika kuingia kwenye Kurasa Zangu na kuthibitisha kwamba bado unaitaka nyumba hiyo.
Sasisha maelezo yako
Unaweza kusasisha maelezo yako ya kibinafsi, kama vile mapato yako na habari za mawasiliano. Hakikisha kuwa tuna anwani yako ya baruapepe na nambari yako ya simu ya mkononi ili tuweze kuwasiliana nawe haraka kuhusu mambo kama kukagua nyumba, ofa na habari zingine muhimu.
Muda na ada ya foleni
Unaweza kuona muda wako wa foleni, yaani, umekuwa kwenye foleni ya nyumba kwa muda gani, katika ukurasa wa mwanzo wa Kurasa Zangu. Unaweza pia kuangalia kama umelipa ada yako ya foleni na wakati ankara ya ada ya mwisho ya foleni ilitumwa.
Waombaji wenza
Unaweza kuongeza mwombaji mwenza, yaani, mtu ambaye unakusudia kuishi naye, kupitia Kurasa Zangu. Manufaa ya kungeza mwombaji mwenza ni kwamba wamiliki wengine wa nyumba wanawaruhusu kuunganisha mapato yenu. Wakati mwingine, mwombaji mwenza anaweza pia kuruhusiwa kuweka jina lake kwenye mkataba.