Shirika la Nyumba la Stockholm – jinsi linavyofanya kazi

Shirika la Nyumba la Stockholm (Bostadsförmedlingen) hufanya kazi kama wakala, likikusaidia kupata nyumba za kukodisha zilizo wazi katika eneo la Stockholm. Nyumba hutolewa kwa msingi wa wakati uliotumika katika foleni ya nyumba. Ili kutuma maombi ya kupata nyumba, lazima kwanza ujisajili katika foleni ya nyumba.

Nani anayeweza kujisajil katika foleni ya nyumba?

Mtu yeyote ambaye ana umri wa miaka 18+ na aliye na namba ya utambulisho wa kibinafsi ya Uswidi (personnummer) au namba ya uratibu (samordningsnummer) anaweza kujiunga na foleni ya nyumba. Unakoishi si muhimu au kama tayari una nyumba. Wakati wako kwenye foleni huanza punde tu baada ya kujisajili, na ukishajisajili unaweza kuanza kutafuta na kuonyesha nyumba unayoipenda. Ada ya foleni ya nyumba ni Krona 200 za Uswidi kila mwaka. 

Aina tofauti za nyumba

Unaweza kutafuta aina tofauti za nyumba na aina za mikataba kupitia Shirika la Nyumba la Stockholm. Ikiwa unasoma katika chuo kikuu au katika elimu ya ufundi wa juu, unaweza kuomba nyumba ya wanafunzi. Ikiwa umri wako ni kati ya miaka 18 na 25, unaweza kuomba nyumba ya vijana. Kuna uwezekano wa kuomba nyumba maalum iliyotengenezwa mahususi kwa wazee ikiwa una umri wa miaka 55+. Mikataba ya muda mfupi hutoa fursa ya makazi ya muda huku ukiendelea kujenga wakati wako wa foleni.

Dhibiti hali

Ni juu yako kutafuta na kuandikisha kuvutiwa kwako na nyumba zilizo wazi zilizotangazwa kwenye tovuti yetu. Matangazo hayo yana habari za kina juu ya makazi hayo, pamoja na masharti ya kupangisha ya mwenye nyumba kwa wapangaji watarajiwa. Ukishaingia kwenye akaunti, unaweza kuandikisha kuvutiwa kwako na nyumba kupitia kwa tangazo hilo. Kumbuka kwamba jinsi unavyotafuta kwa bidii, ndivyo unakavyokuwa na nafasi kubwa ya kupata nyumba.

Inachukua muda gani kupata nyumba?

Muda unaosubiri hutegemea mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na mahali unapotaka kuishi na kiwango cha kodi unachoweza kumudu.

Watu wengi wanaopata nyumba huwa wamesubiri kwenye foleni kwa muda wa kati ya miaka 7 na 11, lakini inaweza kupatikana haraka au kuchukua muda mrefu kuliko huu. Kwa jumla, utahitaji muda mrefu zaidi kwenye foleni ili kupata nyumba iliyo katikati mwa mji au viunga vyake kuliko utakaohitaji kwa nyumba zilizo nje zaidi ya katikati mwa Stockholm.

Pata maelezo zaidi